Tuesday, 8 March 2016

PICHA




PICHA ZA MATUKIO KATIKA PICHA








PITIA HAPA UJISOMEE


Wananchi wa kijiji cha Buchurago kata Bugorora Wilaya ya Missenyi wameiomba serikali ya halmashauri hiyo kukamilisha haraka ujenzi wa barabara inayotoka Bugorora kwenda ktk kijiji hicho ili kuondokana na adha ya usafiri iliyodumu kwa muda mrefu.
Wakizungumza na waandishi wa habari  kwa nyakati tofauti baadhi ya wakazi wa kijiji hicho wamesema kuwa wamekuwa wakitumia usafiri wa Pikipiki tu na kupata shida wakati wa misimu ya mvua.


Wakazi hao wameeleza kuwa tangu kuwepo kwa kijiji hicho hawajawahi kupata barabara bora ya kipita magari ya kubeba abiria hali ambayo wameita usumbufu hasa pale abiria wanapokuwa wengi na mizigo.


Wameongeza  kuwa kukamilika kwa Barabara hiyo itawezesha wenye magari ya kubeba abiria kuanza safari zake kutoka Katika kijiji hicho kwenda Bugorora na Bukoba mjini kwa gharama nafuu kuliko ilivyo sasa.


Aidha wamesema kuwa baadhi ya maeneo unapojengwa barabara hiyo yanajaa maji msimu wa mvua hivyo kuomba mkandarasi kuzingatia hilo ili wasije wakakosa mawasiliano hapo baadae.