Tuesday, 8 March 2016
PITIA HAPA UJISOMEE
Wananchi
wa kijiji cha Buchurago kata Bugorora Wilaya ya Missenyi wameiomba serikali ya
halmashauri hiyo kukamilisha haraka ujenzi wa barabara inayotoka Bugorora
kwenda ktk kijiji hicho ili kuondokana na adha ya usafiri iliyodumu kwa muda
mrefu.
Wakizungumza
na waandishi wa habari kwa nyakati
tofauti baadhi ya wakazi wa kijiji hicho wamesema kuwa wamekuwa wakitumia
usafiri wa Pikipiki tu na kupata shida wakati wa misimu ya mvua.
Wakazi
hao wameeleza kuwa tangu kuwepo kwa kijiji hicho hawajawahi kupata barabara
bora ya kipita magari ya kubeba abiria hali ambayo wameita usumbufu hasa pale
abiria wanapokuwa wengi na mizigo.
Wameongeza
kuwa kukamilika kwa Barabara hiyo itawezesha wenye magari ya kubeba abiria
kuanza safari zake kutoka Katika kijiji hicho kwenda Bugorora na Bukoba mjini
kwa gharama nafuu kuliko ilivyo sasa.
Aidha
wamesema kuwa baadhi ya maeneo unapojengwa barabara hiyo yanajaa maji msimu wa
mvua hivyo kuomba mkandarasi kuzingatia hilo ili wasije wakakosa mawasiliano
hapo baadae.
Subscribe to:
Posts (Atom)










